Wanasiasa na waandishi wa habari wanajiandaa kwa kampeni yenye ushindani mkali Guinea-Bissau

Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari huko Pretoria Aprili 28, 2022. Picha na Phill Magakoe / AFP.

Nchini Guinea-Bissau, mbio za siku 21 hadi Siku ya Uchaguzi zinaanza Novemba 2 na wanasiasa na waandishi wa habari wanajiandaa kwa kampeni yenye ushindani mkali.

Msimu wa uchaguzi wa hali ya juu huleta changamoto za vifaa na maadili kwa wanahabari. Mashirika ya habari yanatayarisha mapendekezo ya utangazaji ya kuwasilisha kwa washirika wa kimataifa, hasa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP).


Mapendekezo haya mara nyingi yanajumuisha maombi ya malipo ya siku, kulipia usafiri, chakula, malazi na mawasiliano kwa wanahabari.
Tabia hii kwa muda mrefu imekuwa ya kawaida nchini Guinea-Bissau, ambapo vyombo vya habari vinakosa rasilimali za kifedha za kuripoti uchaguzi kwa uhuru.

Matokeo yake , wengi watakubali au kugeukia wagombea wa kisiasa au vyama ili kupata usaidizi wa kusafiri, na kutengeneza uhusiano ambao utahatarisha uhuru wa wanahabari. Ili kudumisha kutopendelea, vyombo vya habari vinazidi kutafuta uungwaji mkono kutoka kwenye mashirika ya kimataifa na ya kikanda.