Chama tawala chapendekeza mabadiliko ya katiba yanayopingwa na upinzani nchini Liberia.
Wananchi wa Liberia watakwenda kupiga kura Jumanne kwa ajili ya mapendekezo ya mabadiliko ya katiba ambayo yanaungwa mkono na chama tawala na kupingwa vikali na upinzani.
Moja ya mabadiliko makubwa yaliyo na utata ni mgombea urais anatakiwa awe ameishi nchini humo kutoka miaka 10 hadi 5.
Hiyo itaathiri ni wagombea gani wanaostahili kushiriki uchaguzi ujao. Wanasiasa wengi waliondoka nchini humo wakati wa miaka 14 ya ghasia za kiraia nchini humo ambazo zilimalizika 2003.
Mabadiliko mengine yatachelewesha uchaguzi wa rais kutoka Oktoba mpaka Novemba.Waungaji mkono wanasema hatua hiyo itauondoa uchaguzi wakati wa msimu wa mvua ambapo usafiri unakuwa mgumu sana.