Wivine Kavugho ni mkaazi wa Goma aliye na watoto wa wawili tumekutana nae katika soku kuu ya Virunga Mjini Goma akinunua maharagwe kwa ajili ya familia yake lakini amechanganyikiwa kutokana na bei ambayo hakutarajia.
Esperence Kibwana kwa upande anasema chakula kimepanda bei kutokana na usalama mdogo kwenye vijiji ambako ndipo kuna wakulima ,wengi wao wakishurutishwa kuhama makaazi yao kabla mimea kukomaa.
"Kule maporini hakuna chakula watu wamekimbia kwa sababu ya vita" aliongeza Kibwana.
Lucien Sankara ni muendeshaji boda boda Mjini Goma na mzazi ambaye ameshangazwa kuona kila siku bei ya chakula inapanda.
Wachambuzi wa maswala ya kiuchumi kwa upande wao wakisema hali hii inatokana na vita vya Russia na Ukraine na machafuko yanayo shuhudiwa mashariki mwa Congo makundi ya waasi yakidhiti mashamba ya wakulima anasema Dadi Sale .
Suluhisho ikiwa kwa viongozi kusimamisha machafuko pamoja na vita vya Russia na Ukraine inayopelekea kupanda bei ya mafuta Duniani.
Imetayarishwa na mwandishi wetu Austere Malivika voa Goma.