Raia zaidi ya milioni 40 waliojiandikisha kupiga kura wanakwenda kwenye vituo vya kupigia kura nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuchagua viongazi wao mbalimbali na rais.
Baada ya kampeni za wiki kadhaa, rais Felix Tshisekedi, anagombania muhula mwingine katika uchaguzi ulio na idadi kubwa ya wagombea urais.
DRC kwa sasa inakabiliwa na changamoto mbalimbali lakini hasa usalama upande wa Kaskazini Mashariki, ambapo kuna makundi kadhaa yenye silaha huku kundi la M23 likiendelea kudhoofisha usalama wa eneo hilo.
Kuelekea uchauzi huo, ahadi za kukabiliana na kudhoofu kwa usalama ziligubika kampezi zake, lakini pia masuala mengine kama vile huduma za kijamii ikiwemo afya na hali ya maisha bora kwa raia.
Wananchi wengi waliozungumza na VOA kuelekea uchaguzi wa Jumatano, wametoa ujumbe wa kudumishwa amani.