Kundi hilo la Allied Democratic Forces (ADF), ambalo kundi la Islamic State linadai kuwa ni mshirika wake wa kati kati mwa Afrika, ni mojawapo ya wanamgambo wabaya zaidi mashariki mwa Congo, wanaotuhumiwa kuwaua maelfu ya raia.
Shambulizi la hivi karibuni lilitokea asubuhi ya Jumapili huko Kirindera katika jimbo la Kivu Kaskazini katika eneo la Beni, kulingana na chifu wa kijiji Katembo Kahongya.
"Tuna watu 17 waliofariki na wanne wamejeruhiwa," aliiambia AFP, akiongeza kuwa wanamgambo hao pia wamechoma majengo.
Walitumia silaha za mapanga na moto kuwaua watu," Kahongya alisema.
Aliyekuwa Gavana wa Kivu Kaskazini Carly Nzanzu Kasivita pia alitweet kwamba watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa ADF walikuwa wamewaua watu 19 katika kijiji hicho, akibainisha kuwa idadi hiyo ilikuwa ya muda tu.
Mkazi wa Kirindera, Mukondano Kambale alisema wanamgambo hao waliwaua watu katika hoteli na zahanati ya afya kabla ya kufukuzwa.