Wanamgambo wa Nigeria wauwa wanavijiji

Kina mama na watoto walionusurika shambulizi la Boko Haram katika jimbo la Borno. Jan 31,2013

Mashahidi wanasema wanamgambo hao waliovalia kama wanajeshi, walivamia kijiji cha Lzghe cha jimbo la Bono Jumamosi usiku.
Washambuliaji wanaotuhumiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu wameuwa dazani ya wanavijiji wa Kikristo katika shambulizi kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Mashahidi wanasema wanamgambo hao waliovalia kama wanajeshi, walivamia kijiji cha Lzghe cha jimbo la Bono Jumamosi usiku.

Mamia ya wakazi walilazimika kutoroka eneo hilo wakati washambuliaji walipokuwa wanapora maeneo ya kibiashara na kuchoma moto nyumba kabla ya kuondoka kwa magari waliyoiba.

Maafisa katika eneo hilo na mashahidi wanasema zaidi ya watu 60 waliuwawa. Hapakutolewa dai la haraka juu ya waliohusika na shambulizi hilo, lakini maafisa wa usalama wanashuku kundi la wanamgambo la Boko Haram.

Wiki iliyopita kundi hilo liliuwa wanavijiji 39 katika shambulizi kama hilo kwenye mji mwingine katika jimbo hilo la Bono.