Wanamgambo wa Alshabab wachukua tena udhibiti wa wilaya ya Daynile na kuuwa wanamgambo 60 wa AU.
Mashahidi nchini Somalia wanasema wanamgambo wamechukua tena udhibiti wa maeneo muhimu ya Mogadishu kutoka kwa majeshi ya Umoja wa Afrika.
Waandishi na mashahidi waliiambia VOA kuwa kundi hilo lenye mahusiano na al qaida lilichukua wilaya ya Daynile alhamisi si muda mrefu baada ya maafisa wa Somalia kusema kuwa majeshi yanayoiunga mkono serikali na Umoja wa Afrika yanao udhibiti wa maeneo hayo.
Mashahidi wanasema waliona miili ya wanajeshi wapatao 30 wa umoja wa Afrika . Maafisa wa Alshabab wanasema wapiganaji wao wameuwa wanajeshi wapatao 60 wa Umoja wa Afrika.