Shambulio hilo hatimaye lilizimwa, afisa mmoja katika kambi ya katikati mwa Somalia ya mji wa Galcad aliiambia Reuters. Alisema waliofariki ni pamoja na naibu kamanda wa kambi hiyo, ambaye alikuwa sehemu ya kitengo kilichopatiwa mafunzo na Marekani kilichokuwa hapo.
Shambulio hilo linadhihirisha tishio kubwa la al-Shabaab kwa wanajeshi wa Somalia, hata baada ya mashambulizi ya serikali yaliyoanzishwa mwaka jana kupata mafanikio makubwa dhidi ya wanamgambo wenye uhusiano na al-Qaeda.
Wapiganaji wa Al Shabaab waliivamia kambi ya Galcad mapema siku ya Ijumaa, na kulipua mabomu yaliyotegwa kwenye magari na kufyatua silaha zao, Kapteni Issa Abdullahi alisema.
Kambi hiyo inaendeshwa na Danab, kitengo cha makomandoo waliopatiwa na Marekani ambao wameshiriki katika mashambulizi dhidi ya wanamgambo hao.