Wanajeshi wahukumiwa kwa ubakaji DRC

Wanajeshi wahukumiwa kwa ubakaji DRC

Wanajeshi wahukumiwa kwa ubakaji DRC

Mahakama moja ya kijeshi imewahukumu wanajeshi 9 kwa ubakaji wa halaiki ikiwa ni pamoja na afisa mmoja wa jeshi kwa kuchochea mashambulizi hayo.

Luteni kanali Kibibi Mutware alikutwa na hatia ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na kuhukumiwa miaka 20 jela.

Waendesha mashitaka walimfungulia mashitaka kwa kuamrisha majeshi yake kushambulia wanakijiji katika kijiji cha mashariki cha Fizi siku ya mwaka mpya. Mashahidi wote wanasema wanajeshi hao walibaka zaidi ya wanawake 50 ikiwa ni pamoja na kuiba na kupora mali za wananchi.

Hii inaaminika kuwa ni mara ya kwanza kwa kamanda wa jeshi kuhumukumiwa kwa ubakaji katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.