Mkuu wa jeshi la Ukraine amesema kwamba wanajeshi wa Russia wanaharibu miundo mbinu mashariki na kusini mwa Ukraine.
Vita vya Ukraine vimeingia siku 98.
Wanajeshi wa Russia wanaendelea na mashambulizi ya kuharibu mji wa viwanda wa Sievie-rodo-netsk, ambao waliingia May 27.
Mji wa Sie-viero-do-netsk unatambulika sana tangu utawala wa Kisovieti, na wenye viwanda vikubwa vya kemikali.
Kulingana na gavana wa mji huo, shambulizi la kombora la Russia lilipiga kiwanda kikubwa cha kemikali mjini humo jana jumanne, na kuharibu kabisa tenki la kemikali yenye sumu.
Rais wa Mrekani Joe Biden ametangaza msaada wa roketi za masafa marefu za kukabiliana na makombora ya Russia, pamoja na risasi. Msaada huo ambao ni sehemu ya msaada wa dola milioni 700, unatarajiwa kuwasili Ukraine hii leo.