Wanajeshi wa mwisho wa Ufaransa kuondoka Niger

Wanajeshi wa mwisho wa Ufaransa wanaondoka Niamey

Wanajeshi wa mwisho wa Ufaransa wataondoka Niger na kuashiria mwisho wa zaidi ya muongo mmoja wa operesheni za Ufaransa dhidi ya wanajihadi katika eneo la Sahel huko Afrika Magharibi.

Kuondoka kwa Wafaransa kutoka Niger kunawaacha mamia ya wanajeshi wa Marekani, na idadi ya wanajeshi kadhaa wa Italia na Ujerumani, wakisalia nchini humo.

Ufaransa ilisema itawaondoa takriban wanajeshi wake 1,500 na marubani kutoka Niger baada ya majenerali wapya wa utawala wa lililokuwa koloni la zamani la Ufaransa kuwataka waondoke kufuatia mapinduzi ya Julai 26.

Ilikuwa ni mara ya tatu ndani ya kipindi cha chini ya miezi 18 kwa wanajeshi wa Ufaransa kufunga virago kutoka Sahel.