Kwa mujibu wa vyanzo vya habari doria hiyo ya pamoja ilishambuliwa Jumatano wakati wakiwa kwenye eneo la kusini magharibi mwa Niger.
Wanajeshi waliojeruhiwa walipelekwa Niamey na hali yao ni thabiti maafisa wa Marekani ambao hawakuidhinishwa kuzungumza hadharani walieleza na hivyo kuomba wasitajwe majina. Makomando hao wa kikosi cha Green Berets huenda walishambuliwa katika taifa hilo la Afrika magharibi na wanamgambo wa Al-qaida katika ukanda wa Afrika kaskazini maafisa wameliambia shirika la habari la Associated Press.
Kamandi ya Marekani barani Afrika ilisema makomando wa Marekani wako nchini humo kutoka mafunzo kwa majeshi ya Niger kupambana na wale wenye msimamo mkali katika eneo hilo ikiwemo wale wanaovuka mpaka kuingia Niger kutokea Mali.