Wanajeshi wa Marekani wameanza kuondoka Okinawa Japan

Gavana wa Okinawa Takeshi Onaga, katikati, akiwa ameketi karibu na nakala ya The Ryukyu Shimpo, gazeti kuu la Okinawa, liloripoti maandamano ya ya kupinga kuhamia kwa kambi ya kijeshi ya Marekani mwaka 2015.(AP /Shizuo Kambayashi).

Wanajeshi wa Marekani wameanza kuondoka kidogo kidogo kutoka Okinawa hadi Guam, miaka 12 baada ya Japan na Marekani kukubaliana kuhusu  marekebisho yao ili kupunguza mzigo mkubwa wa kuwepo kwa wanajeshi  wa Marekani katika kisiwa cha kusini mwa Japan.

Uhamaji huo ulianza leo Jumamosi kwa wanajeshi 100 wa Kikosi cha III cha wanajeshi kilichopo Okinawa nak uhamia katika kisiwa \cha Pacifik, Jeshi la Marine la Marekani na Wizara ya Ulinzi ya Japan walisema katika taarifa ya pamoja.

Tokyo na Washington walikubaliana mwaka 2012 kuwahamisha kwa awamu wanajeshi 9,000 kati ya 19,000 wa Marine walioko Okinawa wakiwemo 4,000 hadi Guam.