Wanajeshi wa kikosi maalum cha Afghanistan ambao walipigana pamoja na wanajeshi wa Marekani na kukimbilia Iran baada ya machafuko ya kujiondoa kwa MarekanI wanaajiriwa na jeshi la Russia kupigana huko Ukraine.
Hayo ni kwa mujibu wa majenerali watatu wa zamani wa Afghanistan waliozungumza na The Associated Press.
Walisema Warussia wanataka kuvutia maelfu ya makomandoo wa hali ya juu wa Afghanistan kwa ahadi za malipo ya dola 1,500 kwa mwezi na mahali pa usalama kwa ajili yao na jamaa zao ili waweze kuepuka kufukuzwa nchini humo kwa kile ambacho wengi wanadhania kingekuwa kifo mikononi mwa Taliban.
Jenerali mmoja alisema: "Hawataki kwenda kupigana lakini hawana namna.