Makamu Kamanda wa kikosi cha Afrika Mashariki huko Mashariki mwa Congo Jenerali Emmanuel Kaputa amesema wanajeshi wa Burundi wanapelekwa katika Miji ya Sake Kilolorwe na kichanga wilayani Masisi ambako waasi wa M23 wameombwa kuondoka kuanzia Jumanne tarehe saba mwezi huu na kurudi katika ngome yao ya zamani ya Sabinyo kama njia ya kuheshimu makubaliano ya mkutano wa marais wa Afrika Mashariki uliofanyika Addis Ababa Ethiopia.
“Operesheni hizo zitachukuwa siku kumi wakati ambapo M23 itakuwa ikiondoka katika vijiji walivyo vichukuwa kutoka kwa jeshi la Congo-FARDC lakini bado mapigano yakiendelea Jumapili wakati kikosi hicho kilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Goma" alisema Jenerali Emmauel Kaputa .
Wananchi mashariki mwa Congo wameomba kikosi hicho kukabiliana moja kwa moja na waasi hao la sivyo hatua kali kutoka kwa wananchi zitachukuliwa kwa ajili ya wanajeshi hao wakisema Profesa Balingene Alexi mkuu wa baraza la makabila Kivu Kaskazini ambaye amekutana na viongozi wa operesheni za kijeshi kutoka jeshi la DRC.
Huku Kabila la Wambuti nalo likiwa na msimamo tofauti kuhusu kikosi cha Burundi .
Jumanne waasi wa M23 wameombwa kusimamisha mapigano yao na serikali ya Congo huku wananchi wakisubiri utekelezwaji huo.