Baada ya kutangaza hivi karibuni kwamba kulikuwepo na jaribio la mapinduzi mwezi Februari 2022, Rais Umaro Sissoco Embalo alilivunja bunge la taifa mwezi Mei baada ya kutofautiana na wabunge na kusababisha nchi kukumbwa na msukosuko wa kisiasa.
“Kawaida huwa kunatokea vurugu baada ya kura kuhesabiwa. Lakini wakati huu nina matumaini makubwa kwamba vurugu hazitatokea. Mgombea bora ashinde na amani itawale kote nchini,” Amesema Fode Malam Faty, mwenye umri wa miaka 55, ambaye ni mufuasi wa chama cha Social Renewal (PRS) baada ya kupiga kura yake.
Guinea Bissau, yenye watu milioni 2 , imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa usalama kwa muda mrefu kufuatia mapinduzi ya mara kwa mara tangu ijipatie uhuru kutoka kwa Ureno mwaka wa 1974.