Wanaharakati Kenya wapinga hatua ya serikali kuruhusu bidhaa za GMO

Your browser doesn’t support HTML5

Kuondolewa kwa marufuku ya chakula kilichofanyiwa mabadiliko ya kujenetiki, GMO, kunazidi kuzua hisia kali nchini Kenya leo ikiwa siku ya mashirika ya kijamii kueleza dukuduku lao wakisema soko la Kenya la nje la kuuza bidhaa litaathirika kwa kiasi kikubwa.

Kadhalika wanakosoa kuwa serikali haijawahusisha wadau kutoa maoni yao kabla ya kufanya maamuzi haya.

Matangazo ya Duniani Leo kutoka idhaa ya kiswahili ya Sauti Amerika, Washington, D.C.
#habari