Mwaka 2023, Ethiopia ilizuilia wanahabari 8 kuhusiana na kuripoti ghasia kwenye jimbo la Amhara, kulingana CPJ. Wanahabari hao ni miongoni mwa 320 waliofungwa jela kote ulimwenguni kutokana na kazi zao, CPJ imesema kupitia ripoti yake ya kila mwaka.
Data hizo zinaonyesha idadi ya wanahabari waliozuiliwa kufikia Desemba mosi mwaka jana, wakati mratibu wa CPJ barani Afrika Angela Quintal, amesema kwamba kufungwa jela kwa wanahabari kumeongezeka katika miaka ya karibuni.
Wakati vyombo vya habari vya kimataifa vikielekeza macho yao kwenye vita vya Israel na Hamas, ambapo idadi kubwa zaidi ya wanahabari wameuwawa, wengi hawaangalii mizozo iliyopo kwenye mataifa kadhaa ya kiafrika, ameongeza Quintal.
“Wananchi wa kila taifa wanahitaji kufahamishwa kuhusu kinachoendelea, na wanahabari ni miongoni mwa wale wanaozuiliwa kutokana na kufanya kazi yao,” Quintal ameambia VOA. Nusu ya wanahabari waliozuiliwa Ethiopia walikamatwa kwa tuhuma za kuhujumu serikali, zikiwemo kueneza hofu miongoni mwa umma, kwa nia ya kuendeleza ajenda za kisiasa au kidini.