Maelfu ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Bangladesh waliweka vizuizi kwenye barabara kuu Jumapili, wakidai kukomeshwa kwa viwango vya ubaguzi katika upatikanaji wa kazi za serikali ikiwa ni pamoja na kuhifadhi nafasi za watoto wa mashujaa wa ukombozi.
Wanafunzi takriban wa vyuo vikuu vyote vikuu walishiriki, wakidai mabadiliko ya mfumo wa sifa kwa ajili ya kazi za utumishi wa umma zinazolipa vizuri na zile zenye soko kubwa.
“Ni kufa au kupona kwetu,” mratibu wa maandamano Nahidul Islam ameiiambia AFP, wakati wa maandamano katika Chuo Kikuu cha Dhaka.
Mfumo wa sasa unahifadhi zaidi ya nusu ya nafasi, ambayo ni maelfu ya kazi za serikali.
Hiyo inajumuisha asilimia 30 iliyotengwa kwa ajili ya watoto wa waliopigania uhuru wa Bangladesh mwaka 1971, asilimia 10 kwa wanawake, na nyingine 10 kwa wilaya maalum.