Wanajeshi walipata miili ya waliokufa walipofika shuleni, msemaji wa jeshi Felix Kulayigye alisema katika taarifa.
Kulayigye alisema mapema Jumamosi kwenye Twitter “Jeshi lilikuwa linamsaka adui ili kuwaokoa waliotekwa nyara na kuangamiza kundi hilo.”
Maafisa wa polisi na jeshi wanasema washambuliaji walikua watano na walitia moto bweni baada ya kupora chakula na vitu vingine .
Polisi walisema washambuliaji kutoka kundi la ADF walikimbia kuelekea mbuga ya Virunga nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kituo cha Televisheni cha kibinafsi, NTV Uganda kilisema kwenye Twitter kwamba idadi ya waliofariki ilifikia 41, huku gazeti la serikali la New Vision likisema waliouawa ni 42.
New Vision ilisema 39 kati ya waliofariki ni wanafunzi, na kwamba baadhi ya waliouawa walikufa wakati washambuliaji walipotega bomu wakati wakikimbia.