Wanadiplomasia wa juu wa kundi la G7 wataka mshikamano juu ya China

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Kundi la G7 wakikutana Karuizawa.

Wanadiplomasia wa juu wa kundi la G7 wameanza mazungumzo Japan Jumatatu wakitarajia kuwasilisha ujumbe wa umoja kuhusu wasiwasi wa china baada ya matamshi yenye utata ya rais wa ufaransa Emmanuela Macron.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wana nia ya kuvuka hali iliyosababishwa na matamshi ya Macron kufuatia safari ya Beijing, kwamba Ulaya inapaswa kuepuka migogoro ambayo sio yetu” na China ilikuwa kwenye ajenda hata kabla ya mazungumzo rasmi kuanza Jumatatu asubuhi.

Baada ya kuwasili katika mji wa mapumziko wa kifahari Karuizawa kwa kutumia treni rasmi yenye ulinzi mkali, kundi hilo lilikula chakula cha pamoja huku wakijadili kuhusu China na Korea Kaskaizni huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Yoshimasa Hayashi aliwaambia wenzake kwamba umoja wa G7 ni muhimu sana.

Kikao cha kwanza cha Jumatatu kiliangazia tena changamoto za China na kikanda ambapo Hayashi alianza mazungumzo hayo kwa kuonya jumuiya za kimataifa zilikuwa katika hatua ya mabadiliko ya kihistoria.

Ametoa wito kwa washiriki kuuonyesha ulimwengu dhamira kali ya G7 , kutetea utaratibu wa kimataifa unaozingatia utawala wa sheria.