Wanachama wa Al-Shabaab nchini Somalia ambao hivi karibuni waliapa utiifu wao kwa kundi la kigaidi la Islamic State, wanasogea kuingia mji mkuu Mogadishu. Hayo ni kwa mujibu wa mchambuzi mwandamizi wa maswala ya kijasusi.
Kanali Abdullahi Ali Maow, aliyekuwa afisa wa upelelezi wa kitaifa ambaye sasa anasimamia taasisi mpya ya masuala ya usalama mjini Mogadishu, aliiambia Sauti ya Amerika kwamba baadhi ya wanachama wa Al-Shabaab wanatorokea mji mkuu na maeneo mengine yaliyo karibu na mpaka wa Kenya kwa sababu wamezidiwa nguvu katika mkoa wa Middle Juba.
Maow alisema kwamba Mogadishu inawavutia kwa sababu ni mji ulio na mamilioni ya watu ni sehemu rahisi kujichanganya na watu.