Mashambulizi yametokea katika mkoa wa Balochistan, kusini magharibi mwa Pakistan.
Matukio hayo yametokea katika wilaya za Panjgur na Musakhail ambazo zina idadi ndogo ya watu lakini zinazodhibitiwa na makundi ya wapiganaji.
Polisi wamesema kwamba waasi wameshambulia boboma Panjgur saa sita usiku na kutekeleza mashambulizi ya risasi kabla ya kutoroka wakitumia pikipiki.
Shambulizi la pili limetokea katika kampuni ya kuchimba mafuta ya Musakhail ambapo washambuliaji waliharibu mashine, kufyatua risasi kadhaa na kuteka nyara wafanyakazi 20 kabla ya kutoroka.
Waziri mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif ameamurisha polisi kutumia kila mbinu kuwanasa wahusika. Msako wa maafisa wa usalama unaendelea.