129 wamefariki Nepal baada ya kufunikwa na maporomoko ya ardhi

Mto Bagmati ukiwa umefurika kutokana na mvua nzito Kathmandu, Nepal. Sept 28, 2024

Waokoaji nchini Nepal wamepata darzeni ya mili ya watu kutoka kwenya mabasi na magari mengine, yaliyofunikwa kutokana na maporomoko ya ardhi karibu na mji mkuu wa Kathmandu.

Idadi ya vifo kutokana na mafuriko nchini Nepal, imeongezeka na kufikia watu 129, huku darzani wakiwa hawajulikani walipo.

Hali ya hewa imekuwa bora kiasi leo Jumapili, baada ya mvua ya siku tatu, na shughuli za uokoaji zinaendelea.

Usafiri kuingia na kutoka Kathmandu umeathirika baada ya barabara kuu tatu zinazoingia mjini humo kufungwa na maporomoko ya ardhi.

Serikali imeamurisha shule na vyuo kufungwa kote Nepal kwa muda wa siku tatu.