#VOAElections2020 : Wamarekani washeherekea ushindi wa Rais mteule Biden

Wafuasi wa chama cha Demokratik wakisheherekea baada ya Joe Biden baada ya kutajwa kwamba atakuwa mshindi wa urais Marekani, Jumamosi, Nov. 7, 2020 mjini Washington. (AP Photo/Manuel Balce Ceneta)

Wafuasi wakisheherekea mjini Milwaukee, jimboni Wisconsin, baada ya Joe Biden kutajwa kwamba atakuwa mshindi wa urais Marekani, Jumamosi, Nov. 7, 2020 Nov. 7, 2020, .
 

Wafuasi wa Rais Donald Trump wakishiriki kwenye maandamano ya "Komesha Wizi"  baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa kwamba mgombea Joe Biden ametajwa atakuwa rais, mbele ya bunge la jimbo la Arizona, Phoenix, Marekani Novemba 7, 2020.

Wafuasi wa Rais Donald Trump wamekusanyika nje ya bunge la jimbo ​la Arizona mjini Phoenix Jumamosi, Nov. 7, 2020.

Watu wakisheherekea katika eneo la jirani la Manhattan, jijini New York wakati vyombo vya habari vikitangaza kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Demokratik Joe Biden ametajwa kwamba atakuwa mshindi wa urais, Marekani, November 7, 2020. REUTERS/Andrew Kelly.

Rais wa Marekani Donald Trump akicheza golf katika Klabu ya Taifa ya Golf ya Trump huko Sterling, Virginia, Marekani, Novemba 7, 2020, baada ya matokeo ya urais kutangazwa yakimtaja Joe Biden kwamba atakuwa mshindi wa urais.

Marianne Hoenow wa jimbo la Connecticut akishangilia ushindi wa Rais mteule Joe Biden na Makamu wa Rais mteule Kamala Harris mbele ya Ubalozi wa Marekani Berlin, Ujerumanic Nov. 7, 2020.

Kiongozi wa waliowachache katika Baraza la Seneti Chuck Schumer (D-NY) akisheherekea wakati vyombo vya habari vikitangaza kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Demokratik Joe Biden ametajwa kwamba atakuwa mshindi wa urais, Marekani, November 7, 2020, akiwa mjini Brookly New York , Marekani, Novemba 7, 2020. REUTERS/Dane Rhys

Wafuasi wa Rais wa Marekani Donald Trump wakusanyika nje ya Bunge la Jimbo huko mjini Harrisburg, Pennsylvania, U.S., November 7, 2020 wakati vyombo vya habari vikitangaza kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Demokratik Joe Biden ametajwa kwamba atakuwa mshindi wa urais. REUTERS/Leah Millis 

Wafuasi wa Rais mteule Joe Biden wakisheherekea nje ya White House, Washington, DC Novemba 7, 2020.

Laura Nabors, 33, aliyesafiri kutoka Mississippi, akusanyika na wafuasi wenzake wa Rais wa Marekani Donald Trump nje wakati timu ya wanasheria wakifanya mkutano na waandishi wa habari  baada Joe Biden kutajwa na vyombo vya habari kwamba atakuwa mshindi wa urais uchaguzi wa 2020, huko Philadelphia, Pennsylvania, Marekani. Novemba 7, 2020. REUTERS/Mark Makela

Wafuasi wa Rais mteule Joe Biden na Makamu wa Rais mteule Kamala Harris wakipeperusha bendera huko Las Vegas, Nov. 7, 2020.

Watu wakisheherekea kwenye uwanja wa Times Square, mjini New York baada ya Joe Biden ​kutajwa kwamba atakuwa mshindi wa urais, Novemba 7, 2020.
 

Wafuasi wa chama cha Demokratik wafurahia tangazo la vyombo vya habari kwamba mgombea kiti cha rais wa chama cha Democratic Joe Biden atakuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Marekani wa 2020. Huku wafuasi wa Donald Trump wakiandamana kupinga ushindi huo.