Huku nusu ya nchi ikiwa imelindwakwa kiasi fulani dhidi ya virusi corona, Wamarekani waliepuka vikwazo vya kupambana na virusi hivyo mwishoni mwa juma katika likizo ya siku tatu ambayo kwa kawaida kunakuwa na shamra shamra za kuanza kwa msimu wa joto.
Mwaka mmoja baada ya kujizuia kusafiri kwa ajili ya sikukuu ya mashujaa yaani Memorial Day kupungua kutokana na hofu ya kuenea kwa virusi vya corona, Wamarekani wengi walisafiri kwa ndege na barabara.
Idara inayohusika na utawala wa Usalama wa Usafiri ilisema watu milioni 7.1 walipita katika vituo vya ukaguzi wa usalama kwenye viwanja vya ndege nchini Marekani kutoka siku ya Alhamisi hadi Jumapili.
Ijumaa iliweka rekodi ya siku moja ya juu ya kusafiri watu wengi zaidi tangu Machi 2020, wakati COVID-19 ilipopunguza mahitaji ya kusafiri kwa ndege, kwani watu milioni 1.96 walikaguliwa kwa safari za anga.
Wiki iliyopita, utabiri wa kampuni ya usafiri ya Triple A ulipanda hadi asilimia 60 kwa kipindi cha likizo ya Siku ya Memorial na watu milioni 37 wanatarajiwa kusafiri kilomita 80 au zaidi kutoka nyumbani kwao Triple A ilisema.