Wamarekani waamua kati ya Trump na Biden

Rais Donald Trump na aliyekuwa makam wa rais Joe Biden

Wamarekani wanapiga kura hii leo kumchagua rais atakayeongoza taifa hilo kubwa zaidi kiuchumi duniani kwa mda wa miaka minne ijayo.

Rais wa sasa Donald Trump anatetea nafasi hiyo kupitia chama cha Republican huku aliyekuwa makam wa rais Joe Biden akigombea kupitia chama cha Democratic.

Kufikia jana jumatatu, karibu wapiga kura milioni 100 walikuwa tayari wamepiga kura katika uchaguzi huo.

Kura zimepigwa kwa njia ya posta na kwa njia ya kawaida ya mpiga kura kufika katika kituo cha kupigia kura.

Jaribio la warepublican kutaka kura 127,000 zilizopigwa na wapiga kura waliofanikisha zoezi hilo wakiwa kwenye magari yao katika vituo vya kupigia kuwa, zisihesabiwe, lilikataliwa na mahakama katika jimbo la Texas.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC