Mapigano yauwa 600 Darfur mwezi Mei.

Wakimbizi wa Darfur.

Walinda amani wa kimataifa wanasema mapigano katika eneo la Darfur yameuwa karibu watu 600 wakati wa mwezi Mei ikiwa ni idadi kubwa kuliko zote ya mauaji katika zaidi ya miaka miwili.

Walinda amani wa kimataifa wansema mapigano katika eneo la Darfur yameuwa karibu watu 600 wakati wa mwezi Mei ikiwa ni idadi kubwa kuliko zote ya mauaji katika zaidi ya miaka miwili.

Maafisa wa wa AU huko Darfur wanasema idadi ya waliokufa ilikuwa ni kubwa iliyoorodheshwa tangu walinda amani walipopelekwa January 2008.

Idadi ya waliojeruhiwa iliyotolewa jumatatu iliunganisha vifo kutoka kote kwenye ghasia kati ya makundi ya waasi ya Darfur na serikali ya Sudan.

Mapigano mapya kati ya serikali na kikosi cha waasi cha Justice and Equality Movement yalianza upya mwezi Mei baada ya JEM kutoka kwenye kikao cha mapatano ya amani huko Qatar.