Wakulima wamewasha moto nje ya jengo la bunge la ulaya mjini Brussels leo Alhamisi kama sehemu ya maandamano yanayoendelea kufuatia gharama kubwa, kanuni na ukiritimba.
Malalamiko yalipangwa kusikilizwa na viongozi wa EU katika mkutano huo baadae hivi leo, kwenye eneo tofauti ambako maandamano yanafanyika.
Waandamanaji waliwasha moto kwenye lundo la nyasi, huku maafisa wa zimamoto walijaribu kuzima.
Hiyo ni baada ya wakulima kuingia katika mji mkuu wa Ubelgiji wakiwa na matrekta makubwa nyakati za asubuhi – ikiwa ni kilele cha wiki kadhaa za maandamano kuzunguka umoja huo.
Hata wakati ambapo Mkutano wa EU ulitakiwa kuzingatia zaidi kutoa msaada wa kifedha kwa Ukraine kwa vita vyake dhidi ya uvamizi wa Russia, wakulima walitaka kuingiza agenda isiyo rasmi kwa viongozi 27 wa umoja huo.