Baadhi ya wabunge walivitaja vita vya Russia dhidi ya Ukraine na ukandamizaji wa haki za binadamu nchini Iran kama sababu za kususia kwao.
Wakfu wa Nobel ulibatilisha mwaliko wake kwa wawakilishi wa Russia, Belarus na Iran kuhudhuria sherehe za mwaka huu za tuzo ya Nobel baada ya uamuzi huo wenye utata kuibua majibu kali.
Kubatilishwa huko siku ya Jumamosi kulikuja baada ya wabunge kadhaa wa Sweden kusema kwamba watasusia sherehe za mwaka huu za tuzo ya Nobeli baada ya taasisi hiyo binafsi inayosimamia tuzo hizo za kifahari kubadilisha msimamo wake kutoka mwaka mmoja uliopita na kuzikaribisha nchi hizo tatu kuhudhuria.
Baadhi ya wabunge walivitaja vita vya Russia dhidi ya Ukraine na ukandamizaji wa haki za binadamu nchini Iran kama sababu za kususia kwao.