Ghadhabu zimeongezeka nchini Kenya kutokana na kupanda kwa bei ya chakula na bidhaa nyingine za msingi.
Wakenya wameendelea kuelezea hisia zao kwenye mitandao ya kijamii, wakiitaka serikali kuchukua kila hatua na kupunguza bei ya chakula.
Baadhi ya watu wamekuwa wakichapisha risiti zao baada ya kununua vyakula, ili kuonyesha namna bei za bidhaa kama mafuta ya kupikia, na mkate zilivyopanda bei katika muda wa miaka mitatu, huku baadhi ya zikiwa zimepanda bei mara mbili au tatu zaidi.
Wanaishutumu serikali kwa kushindwa kudhibithi ongezeko la bei.
Kodi za juu na gharama kubwa za uzalishaji ni miongoni mwa sababu zilizotajwa kupelekea bei kupanda.
Shirika la takwimu nchini Kenya limesema kwamba mfumuko wa bei umepanda kwa asilimia 8.89 mwezi Januari.