Waziri wa mambo ya kigeni wa Congo Jean Claude Gakosso katika mawasiliano kwa njia ya simu na shirika la habari la AFP amesema kwamba ujumbe huo utakusanya taarifa pamoja na kuhakikisha kwamba mchakato kuelekea zoezi hilo unaendelea vyema.
Waziri huyo ameongeza kusema kwamba wajumbe wa AU watakutana na viongozi wa kisiasa, viongozi wa kidini,pamoja na washikadau wengine kwenye miji ya Tripoli, Benghazi, Tobruk na Misrata.
Wajumbe hao pia wanatarajiwa kukutana na raia wa Libya wanaoishi Misri pamoja na Tunisia. Baada ya kukamilisha ziara yao, wajumbe hao watarejea Brazzaville ili kumfahamisha Nguesso kuhusiana na hali halisi kabla ya kuhudhuria kongamano la Novemba 12 kuhusiana na Libya nchini Ufaransa.
Rais huyo mwezi Julai alikutana na kiongozi wa Libya Mohamed al Menfi nchini mwake ili kuzungumzia mipango ya uchaguzi. Libya ilitumbukia kwenye machafuko mwaka wa 2011 baada ya kuondolewa kwa dikteta wa muda mrefu Moamer Kadhafi, na licha ya nchi hiyo kuwa na utajiri mkubwa wa mafuta, watu wengi wangali wanaishi kwenye hali ya umaskini.