Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, hayo yanajiri wakati ambapo Israel inaendelea na mashambulizi yake makubwa ya mwezi huu kusini mwa Gaza.
Qatar, Marekani na Misri zimekuwa zikiongoza juhudi za upatanishi kati ya pande zote kwa wiki kadhaa juu ya kuachiliwa mateka kwa mabadilishano ya kusitisha mapigano , kuachiliwa wafungwa wa Palestina na misaada zaidi katika kanda hiyo.
Lakini mpango huo umezuiwa , vyanzo vya habari vimesema , kutokana na kwamba Hamas na Israel wana tofautiana juu ya jinsi ya kumaliza kabisa vita katika ukanda wa Gaza.
Maafisa wa Qatar na misri hawajatoa maelezo yeyote kufuatia maombi ya Reuters. Ingawa white House ilithibitisha kwamba mjumbe wa mashariki ya kati Brett McGurk alikuwa Cairo kwa mazungumzo yanayoendelea, kuhusu kuachiliwa mateka na msaada ingawa alikataa kutoa maelezo kuhusu ripoti ya makubaliano yoyote ya sitisho la mapigano.