Ubalozi wa China, jijini Tokyo, Japan, Jumapili umetangaza kwamba utaanza kutoa visa kwa raia wa Japan.
Hatua hiyo inamaliza hatua ulipizaji kisasi dhidi ya uamuzi wa Japan uliotaka kupimwa Covid kwa wasafiri wanao wasili kutoka China bara, ambako idadi ya maambukizi inaongezeka.
Taarifa fupi iliyowekwa mtandaoni imesema kuanzia Jumapili, ubalozi na ofisi ndogo za kibalozi za serekali ya watu wa China zitaanza kutoa visa za kawaida kwa raia wa Japan.
China ilisimamisha kutoa viza kwa raia wa Japan toka Januari 10 baada ya Tokyo kuanza kuwataka watu kutoka China bara kupima Covid kabla ya kusafiri na watakapo wasili.
China pia ilisimamisha kutoa viza kwa Wakorea Kusini kwa sababu kama hizo mapema mwezi huu. Ubalozi wa China, Korea Kusini haijaondoa maharti hayo mpaka ilipofika Jumapili jioni.