Waislam duniani washeherekea Idd El Fitr

Kinamama wa Kiislam wakiadhimisha swala ya Idd huko , Colorado.

Waislam duniani wanasherehekea Idd El Fitr ikiwa ni mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan

Waislam duniani wanasherehekea Idd El Fitr ikiwa ni mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan .

Huko Mashariki ya kati zaidi ya watu elfu 30 huko Syria walivuka mpaka kutoa salaam za Idd kwa ndugu zao katika nchi jirani ya Uturuki.

Kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei aliadhimisha sherehe hizo kwa kukosoa Israel kwa kile alichokiita ukandamizaji wa wapalestina . Katika swala ya Ijumaa huko Tehran pia aliishutumu Marekani na mataifa mengine ya Magharibi kwa kuhusika na ukandamizaji wa wapalestina.

Alhamisi Rais wa Marekani Barack Obama alituma salaam za Idd kwa waislam wote duniani katika sikukuu ya Idd El Fitr kuadhimisha kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Katika taarifa yake alisema wakati huu wa sikukuu ni wakati wa kutafakari na kuangalia amani ambazo waislam na watu wa dini nyingine wanatambua.