Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kupitia ripoti wanasema, waasi wa Kihothi wa Yemen, wamebadilika kuwa taasisi yenye nguvu ya kijeshi ikipata msaada kutoka Iran, makundi ya Iraq, na wanamgambo wa Hezbollah wa Lebanon.
Kundi hilo limetumia mgogoro wa Israel na Hamas, wa Gaza, kujiongezea hali yao katika kile ilichojieleza kuwa “Mpango wa Kupinga” kujipatia umaarufu katika ukanda huo na kweingineko wamesema wataalamu wanaoangalia vikwazo dhidi ya Wahothi, kupitia ripoti yenye kurasa 537 kwenda Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Kusaidia wanamgambo hao wanaoungwa mkono na Iran, wa Hamas, ambao walifanya shambulizi la kushtukiza Oktoba 7, 2023, na kuzusha vita vya Gaza, Wahothi wamekuwa wakishambulia meli katika bahari ya Sham na Ghuba ya Aden, ambapo wamesumbua usafirishaji duniani wa bidhaa na maeneo muhimu ya kikanda.