Miili miwili ilipatikana na wahamiaji 178 waliokolewa wakati wa operesheni tatu kwenye pwani ya kusini mwa Tunisia, taarifa ya wizara ya ulinzi imesema.
Wizara hiyo imesema wahamiaji hao ambao ni kutoka Misri, Tunisia, Syria, Ivory Coast, Bangladesh, Nigeria, Mali na Ethiopia, walikuwa wameondoka kutoka bandari ya Libya ya Zuwara Ijumaa usiku.
Alhamisi, viongozi wa Tunisia walikamata wahamiaji 267 ambao walikua wameanza kuvuka bahari kutoka Libya, wengi wao wakiwa raia wa Bangladesh, shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, limesema.
Kwa mujibu wa na takwimu za IOM, zaidi ya wahamiaji elfu 1 waliotarajia kufika Ulaya walikuwa wameondoka Libya na kuishia Tunisia tangu mwezi Januari, na idadi ya wanaoondoka inazidi kuongezeka.
Imetarishwa na Harrison Kamau