Walinzi wa pwani ya Uhispania wamewaokoa darzeni ya wahamiaji kutoka visiwa vya Canary leo Jumatano.
Walinzi hao waligundua boti tano za mbao karibu na visiwa vya Canary.
Wanaume 60 na wanawake 4 wameokolewa kutoka kwenye boti hizo.
Maafisa wa huduma za dharura wamesema kwamba boti nyingine tatu zilizotengenezwa kwa mbao ziligunduliwa karibu na El Hierro na nyingine ilikuwa imebeba zaidi ya wahamiaji 40 karibu na kisiwa cha Tenerife.
Sehemu hiyo imeshuhudia ongezeko la wahamiaji wanaowasili kwa njia ya bahari katika Umoja wa Ulaya mwaka huu.
Wizara ya mambo ya ndani ya Uhispania imesema kufikia Desemba 15, jumla ya wahamiaji 43,737, ikiwa ni zaidi ya asilimia 18.6 wamewasili Uhispania mwaka huu.