Maafisa wanasema boti ndogo iliyokuwa imebeba wahamiaji katika njia ya maji ya Uingereza ilizama Jumamosi, na watu sita walifariki. Watu wengine wawili walipotea, maafisa hao wamesema.
Takriban watu 65 wanaaminika walikuwa ndani ya boti hiyo ilipoanza kuzama.
Meli iliyokuwa ikipita iliwatahadharisha maafisa mapema Jumamosi kuhusu boti hiyo iliyokuwa imebeba watu wengi kupitia kiasi nje ya pwani ya Calais, na kusababisha majibu kutoka kwa walinzi wa pwani wa Uingereza na Ufaransa.
BBC iliripoti kwamba watu sita waliofariki ni wanaume raia wa Afghanistan.
Maafisa wa Uingereza na Ufaransa walishindwa kuzuia wimbi la watu wanaotafuta hifadhi ambao wako tayari kufanya safari hatari kwenda Uingereza kwa kutumia boti zisizokuwa salama.