Timu za uokoaji ziliopoa miili ya watu 17, akiwemo mtoto mchanga, na watu 25 waliokolewa, waziri mkuu wa Bahamas Philip Davis aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.
Davis alisema maafisa wanaamini watu hao walikuwa kwenye boti ya mwendo kasi kuelekea Miami.
“Inaaminika kuwa boti hiyo ilizama kwenye bahari iliyochafuka”, amesema.
Hadi watu 60 walikuwa kwenye boti hiyo na watu zaidi wanahofiwa kutoweka, Kamishna wa polisi Clayton Fernander amesema.
Maafisa wa Bahamas wamesema watu wawili wamekwa mbaroni, wote ni kutoka Bahamas, wakishukiwa kufanya usafirishaji haramu wa binadamu. Watu wote waliokuwa kwenye boti ambao waliokolewa au kufariki au waliotoweka wanaaminika kuwa wahamiaji kutoka Haiti.
Waziri wa idara ya uhamiaji Keith Bell amesema manusura walieleza kuwa walilipa kati ya dola 3,000 na dola 8,000 kwa safari hiyo.