Katika taarifa ya pamoja, wagombea hao wameahidi kushirikiana ili kuzuia uchakachuaji wowote wa matokeo na kuitaka tume ya uchaguzi kuchukua hatua kadhaa, ikiwemo kuchapisha orodha ya wapiga kura na ramani ya vituo vya kupigia kura.
Kumekuwa na hali ya mvutano kabla ya uchaguzi wa tarehe 20 Desemba. Washirika wa kimataifa na makundi ya haki za binadamu yamezishtumu mamlaka kukandamiza wapinzani na uhuru wa kujieleza, madai yaliyokanushwa na serikali.
Wagombea wote wa upinzani wameelezea wasiwasi wao juu ya uwezekano wa wizi wa kura na ukosefu wa uwazi.
“Baada ya utata mwingi na ukosefu wa umakini ambao uligubika shughuli zote za kabla ya uchaguzi, ni muhimu siku chache kabla ya kampeni ya uchaguzi, hatua za haraka zichukuliwe kuokoa mchakato wa uchaguzi,” taarifa yao imesema.