Wafuasi wa MRC wadai kuandamwa na serikali

Wafuasi wa kundi la MRC mjini Mombasa

Vyombo vya usalama nchini Kenya vimeanza kuwaandama tena viongozi wa vuguvugu la Mombasa Republican Council –MRC kundi ambalo limekuwa likishinikiza agenda ya pwani kujitenge kutoka Jamhuri ya Kenya.

Wafuasi wa kundi hilo nao wanadai serikali inawahangaisha, siku chache baada ya polisi wa Kenya kusema MRC inawasajili wanachama wapya wakiwemo wanawake.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Josephat Kioko wa Mombasa, kenya

Mvutano huu sio mpya ndani ya vyombo vya usalama nchini Kenya na vuguvugu la Mombasa Republican Council- MRC anghlabu ndani ya kipindi cha miaka 10 iliyopita ndani ya mwezi mmoja viongozi kadhaa na wafuasi wengine wa kundi hilo wamekamatwa na kushtakiwa na polisi katika maeneo ya pwani kutokana na mikutano ambayo polisi wanaitaja kama sio mikutano halali.

Wafuasi hao hivi sasa wanaitaka mahakama ya juu zaidi nchini humo kuweka wazi suala la uhalali wa vuguvugu la MRC ambalo wakati mmoja liliishitaki serikali kwa kuwajumuisha kuwa miongoni mwa makundi haramu.