Maafisa nchini Pakistan wanasema vifo kutokana na mafuriko yaliyoenea vimefikia 1,000 tangu katikati ya mwezi wa Juni na waziri wa hali ya hewa wa nchi hiyo aliuita msimu mbaya wa monsoon na "janga kubwa la hali ya hewa."
Mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa yamesomba vijiji na mazao huku wanajeshi na waokoaji wakiwahamisha wakaazi waliokwama hadi katika kambi za misaada na kutoa chakula kwa maelfu ya raia wa Pakistani waliokimbia makazi yao.
Mamlaka ya Kitaifa ya Kudhibiti Maafa nchini humo iliripoti Jumapili idadi ya vifo tangu msimu wa mvua za masika kuanza mapema kuliko kawaida mwaka huu katikati ya Juni ilifikia watu 1,033 baada ya vifo vipya kuripotiwa katika majimbo ya Khyber Pakht-unkhwa na kusini mwa Sindh.