Wademokrat na Warepublikan njia panda kufungwa serikali.

Bunge la Marekani.

Huku siku ya mwisho ikiwa imekaribia hapo Ijumaa usiku kabla ya kuwa na uwezekano wa kufungwa kwa shughuli za serikali ya Marekani wabunge wa vyama vya democrat na republican wako njia panda kukubaliana ili shughuli za serikali ziendelee bila ya kuweka hatarini mambo yalio na kipaumbele kwa vyama vyao.

Wademokrat wanataka muswaada wa kujitegemea ili serikali iweze kuendelea kufanya kazi wakati kwa upande wa chama cha republican wanataka muswaada uliounganishwa na usalama wa mipaka na mabadiliko ya uhamiaji.

Warepublikan waliwatumia wademokrat muswaada ambao hauna sera ya kuwalinda wahamiaji laki 7 wasio na vibali walioletwa nchini na wazazi wao wakiwa watoto wadogo lakini inawapa nafasi wademokrat hatua ya kipaumbele cha juu ya kurudisha tena bima ya afya kwa watoto kwa miaka sita. (CHIP).