Duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Colombia yafanyika

Wapiga kura washiriki duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Colombia.

Wapiga kura nchini Colombia Jumapili wanachagua kati ya muasi wa zamani, na milionea asiyetabirika katika duru ya pili ya kura ya urais ambayo inaahidi kuleta taswira mpya ya nchi hiyo baada ya uchaguzi wa duru ya kwanza kutompata mshindi wa wazi.

Kura za maoni zinaonyesha mwanasiasa wa mrengo wa kushoto, Gustavo Petro, na mpinzani wake, Rodolfo Hernández - wote mameya wa zamani – wanana uungwaji mkono sawa, tangu kuwashinda wagombea wengine wanne katika uchaguzi wa awali wa tarehe 26 mwezi Mei ambapo hakuna aliyepata kura za kutosha kushinda moja kwa moja, na hivyo kulazimisha duru ya pili.

Takriban watu milioni 39 wanlitarajiwa kupiga kura loe Jumapili, lakini takwimu zinaonyesha kwamba, katika kila uchaguzi wa urais tangu mwaka wa 1990, zaidi ya asili mia 40 wamekuwa hawashiriki uchaguzi.

Raia wa Colombia wanapiga kura huku kukiwa na hali ya kutoridhika iliyoenea juu ya kuongezeka kwa ukosefu wa usawa, mfumuko wa bei na ghasia.

Wengi wameonyesha kutoridhika na hali ya nchi hivi kwamba katika duru ya kwanza waliwaondoa wanasiasa wa muda mrefu na wanaoegemea upande wa kulia, na kuchagua watu wawili ambao hawana historia ndefu ya siasa.