Wachimba migodi watatu wafariki nchini Zimbabwe

Wachimba migodi wapiga pichwa kwenye mgodi wa dhahabu wa Freda Rebecca katika mji wa Bindura, Februari 7, 2015. Picha ya Reuters

Wachimba migodi watatu walifariki na wengine 18 wanahofiwa kuzikwa baada ya shimo katika mgodi wa dhahabu usio rasmi nchini Zimbabwe kuporomoka, televisheni ya serikali imesema Jumamosi.

Ajali hiyo ilitokea siku ya Ijumaa huko Chegutu, umbali wa kilomita 120 na mji mkuu Harare, kituo cha televisheni cha ZBC kimesema.

Kilisema “Miili mitatu iliondolewa kweye mgodi ulioporomoka wa Bay Horse huko Chigutu.”

Taifa hilo la Kusini mwa Afrika lina akiba kubwa ya madini ya platinamu, alimasi, dhahabu na shaba. Lakini kutokana na uchumi unaodorora, uchimbaji haramu wa madini umekithiri na mara nyingi hufanyika katika hali ya hatari