Wabunge wa Marekani wanatarajiwa kupiga kura Jumanne kwa ajili ya muswada wa kupitisha msaada wa dola bilioni 33 kwa Ukraine kwa ajii ya masuala ya kijeshi na kibinadamu.
Kabla ya kuelekea katika kura za baraza la wawakilishi, rais wa Marekani, Joe Biden amesema utawala wake umekaribia mwisho wa mamlaka yake ya kupeleka silaha na vifaa vingine vya kijeshi kutoka katika hifadhi ya Pentagon.
Waziri wa mambo ya nje Antony Binken, na waziri wa ulinzi Lloyd Austin walitoa mwito wa pamoja kwa wabunge, wakiwasihi kuchukuwa uamuzi huo kabla ya Mei 19 ambapo wanatarajia msaada wa sasa utakwisha.
Kiongozi wa walio wachache katika seneti Mitch McConnel, Jumatatu alisema kwamba wakati juhudi mpya zikifikiriwa, kuna mabadiliko ya mchakato yanayotakiwa kufanyika, lakini anatarajia suala hilo kushughulikiwa haraka.