Ukeketaji umepigwa marufuku Gambia toka mwaka 2015, lakini mila hiyo iliyokita mizizi bado imeenea katika taifa hilo la Afrika Magharibi na hukumu za kwanza mwaka jana zilichochea upinzani dhidi ya sheria hiyo.
Baada ya mjadala mkali Jumatatu, mapendekezo yaliyomo katika ripoti ya kamati ya pamoja ya afya na jinsia yaliidhinishwa na kikao cha bunge, huku wabunge 35 wakipiga kura ya kuunga mkono kupitishwa kwa ripoti hiyo, 17 wakipinga na wawili hawakuhudhuria.
Kura ya mwisho kuhusu mswada wa kuharamisha ukeketaji kwa sasa imepangwa kufanyika Julai 24.
Iwapo bunge litaiidhinisha, Gambia itakuwa nchi ya kwanza kubatilisha marufuku ya ukeketaji.
Ilipitisha usomaji wake wa pili mwezi Machi na wabunge watano tu kati ya 53 walipiga kura dhidi yake na mmoja kutoshiriki.