Wabunge hao walivutana vikali walipoanza kutathmini hoja iliyopitishwa siku iliyotangulia na kamati ya maandalizi, ikipendekeza kucheleweshwa uchaguzi kwa miezi sita au hata hadi kufikia mwezi Februari 2025, kulingana na hati iliyosambazwa kwenye mkutano huo.
Wafuasi wa Karim Wade, ambaye azma yake ya kuwania urais ilikataliwa na Baraza la Kikatiba waliwasilisha pendekezo hilo.
Hati hiyo ikisema kuwa lengo la kuahirishwa kwa uchaguzi huo itakuwa “ni kuepusha mzozo wa kiutawala na machafuko makubwa ya kisiasa” na kuhakikisha “kurejeshwa kikamilifu kwa mchakato wa uchaguzi”
Hati hiyo inaungwa mkono na kambi ya wabunge ya Rais Sall.
Nje ya jengo la bunge maafisa wa usalama walitumia mabomu ya kutoa machozi kuutawanya mkutano wa upinzani siku ya Jumatatu, muda mfupi kabla ya kuanza kwa mjadala huo wenye utata wa uahirishwaji wa uchaguzi wa rais wa mwezi huu.
Waandamanaji kadhaa walisikika wakiimba “Macky Sall dikteta” wakimaanisha rais aliyeko madarakani baada ya kutawanywa na maafisa wa usalama.
Wafuasi wa Karim Wade, ambaye azma yake ya kuwania urais ilikataliwa na Baraza la Kikatiba iliyowasilisha pendekezo hilo.
Hati hiypoiIkisema kuwa lengo la kuahirishwa kwa uchaguzi huo ni “kuepusha mzozo wa kiutawala na machafuko makubwa ya kisiasa” na kuhakikisha “kurejeshwa kamili kwa mchakato wa uchaguzi”.
Hati hiyo inaungwa mkono na kambi ya Rais Sall.
Nje ya jingo la bunge, vikosi vya usalama vilitumia mabomu ya kutoa machozi kuutawanya mkutano wa hadhara siku ya Jumatatu , muda mfupi kabla ya ya kuanza kwa mjadala mkali kuhusiana na uahirishwaji wa mwezi wa uchaguzi.
Senegal imekumbwa na mzozo wa kisiasa tangu Rais Sall kutangaza kuchelewesha uchaguzi huo wa rais siku ya Jumamosi, masaa machache kabla ya kampeni kuanza rasmi.
Viongozi wa upinzani wameilaani hatua hiyo na kusema ni “mapinduzi ya kikatiba”, wakisema ni ukandamizaji wa demokrasia.
Siku ya Jumatatu, mawasiliano ya mtandao wa simu yalisitishwa katika wilaya kadhaa za mji mkuu wa Dakar, kulingana na raia na waandishi habari.
Serikali pia ilisitisha data za simu mwezi Juni mwaka jana kutokana na mvutano mkubwa nchini humo. Hatua hiyo imekuwa jibu la kawaida la kuzuia uhamasishaji na mawasiliano kupitia mitandao ya kijamii.
Hali hiyo imezua wasiwasi mkubwa katika jumuiya ya kimataifa, huku Marekani, Umoja wa Ulaya na mtawala wa zamani wa kikoloni Ufaransa wakiomba kura hiyo kupangwa upya haraka iwezekanavyo.
Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat, Jumatatu aliitaka Senegal kutatua mzozo wake wa kisiasa kwa mashauriano, maelewano na mazungumz, baada ya makabiliano makali kuzuka kufuatia kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais wa mwezi huu.
Faki alitoa wito kwa maafisa wa serikali kuandaa uchaguzi haraka iwezekanavyo, kwa uwazi, kwa amani na utangamano wa kitaifa katika taarifa kwenye mtandao wa X. baada ya Rais Macky Sall kutangaza kuwa uchaguzi wa Februari 25 umeahirishwa kwa muda usiojulikana.