Kamati ya kulinda waandishi wa habari CPJ inasema asilimia 95 ya waandishi wa habari waliouwawa duniani katika miaka 10 iliyopita walikuwa ni waandishi wa habari wa ndani ya nchi. Zaidi ya hayo katika ripoti yake mpya inaeleza kwamba wengi waliotenda maovu hayo hawajaadhibiwa.
CPJ inasema tabia hiyo ya kutoadhibiwa ni moja ya vitisho vikubwa kwa uhuru wa vyombo vya habari . Mshauri wa CPJ Elizabeth Witchel ambaye pia ni mwandishi wa kitabu cha Global Impunity Index kiitwacho “Getting away with Murder” anasema Sudan Kusini ni moja kati ya nchi 5 za juu ambako waandishi wa habari katika idadi ya waandishi wa habari waliouwawa bila mtu yeyote kushitakiwa 2016.
Bi Witchel amesema hali ni ya hatari sana, hatari kuliko wakati mwingine wowote ule, ambapo wanashuhudia waandishi wa habari wakilengwa si kwa kazi yao tu, bali tu kwasababu ni waandishi wa habari “.